Kazi za Mamlaka zimeainishwa katika kifungu cha tano (5) cha Sheria Na. 3 ya LATRA ya Mwaka 2019 kama ifuatavyo;
(a) Kutekeleza majukumu ya Sheria za Kisekta;
(b) Kutoa, kuhuisha, au kufuta leseni za usafirishaji;
(c) Kwa kuzingatia matakwa ya sheria za Kisekta-
(i) Kusimamia viwango vya ubora wa huduma na usalama katika sekta zinazodhibitiwa;
(ii) Kuweka vigezo na masharti ya utoaji wa huduma zinazodhibitiwa; na
(iii) Kudhibiti viwango vya tozo za huduma;
(d) Kuratibu shughuli za usalama wa usafiri ardhini;
(e) Kusajili wahudumu na kuthibitisha madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ardhini;
(f) Kuhakikisha na Kuthibitisha hali ya usalama wa vyombo vya usafiri wa umma ardhini kwa matumizi;
(g) Kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa sekta zinazodhibitiwa kwa kuangalia viwango vya uwekezaji, gharama, upatikanaji na ufanisi wa huduma
(h) Kushughulikia na kuwezesha utatuzi wa migogoro na malalamiko ;
(i) Kuelimisha umma kuhusu kazi na wajibu wa Mamlaka