Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kurugenzi ya Udhibiti Usafiri wa Barabara

Kazi

Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;

  • Kukuza ushindani na kuzuia ukiritimba katika sekta ndogo ya usafiri wa barabarani;
  • Kuandaa na kupitia Sheria na Kanuni za huduma za usafiri wa barabara;
  • Kutoa msaada kiufundi kwa uandaaji wa taratibu na viwango;
  • Kusimamia utoaji wa leseni na/au usajili wa vyombo vya moto kibiashara kwa kuzingatia mahitaji ya udhibiti;
  • Kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni na viwango kwa vyombo vya moto kibiashara;
  • Kuunda na kupitia upya kanuni za maadili kwa watoa huduma na watumiaji wa huduma za usafiri wa barabara kibiashara;
  • Kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na Wizara yenye dhamana ya usafiri kwenye masuala yanayohusu usafiri ardhini; na
  • Kuratibu huduma za usafiri wa mipakani.
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo