Idara inatekeleza majukumu yafuatayo;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni pamoja na vibali vya magari ya kibiashara;
- Kutoa vibali vya kuruhusu usafiri kuvuka nje ya mipaka;
- Kuandaa na kupitia kanuni na viwango vya magari ya kibiashara;
- Kukuza ushindani na kuzuia ukiritimba kwa wasafirishaji wenye nguvu katika sekta ndogo ya usafiri wa barabara;
- Kutayarisha ratiba ya mabasi na ya abiria;
- Kuanzisha na kupitia njia za magari ya abiria;
- Kutengeneza kanuni za maadili kwa watoa huduma, madereva na wafanyakazi; na
- malalamiko migororo ya wateja yanayohusiana na utoaji leseni