Idara inatekeleza kazi zifuatazo;
- Kuainisha maeneo ya mafunzo na utafiti na kupendekeza athari za kiudhibiti katika sekta ndogo za usafiri ardhini zinazodhibitiwa;
- Kutathmini utendaji kazi wa sekta ndogo zinazodhibitiwa;
- Kuanzisha mahitaji na usambazaji wa huduma zinazodhibitiwa;
- Kuratibu utengenezaji wa vigezo/viwango vya utendaji wa huduma zinazodhibitiwa;
- Kukusanya taarifa na data kuhusu kanuni na taratibu bora za kiudhibiti katika taasisi zinazoshabihiana;
- Kutengeneza viashiria vya utendajikazi na vigezo vya sekta ndogo zinazodhibitiwa;
- Kuratibu utayarishaji wa taarifa za utafiti na machapisho;
- Kushirikiana na watoa huduma kwenye masuala muhimu yanayohusu udhibiti uchumi;
- Kukusanya, kuchambua na kutafsiri data na taarifa zilizokusanywa kutoka sekta ndogo zinazodhibitiwa; na
- Kusanifu na kuhifadhi mifumo ya usimamizi wa data kuhusu taarifa zilizokusanywa kutoka kwa sekta ndogo zinazodhibitiwa