Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kurugenzi ya Udhibiti Usafiri wa Reli

Kazi 

Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;

 • Kukuza ushindani na kuzuia ukiritimba katika sekta ndogo ya reli;
 • Kutoa, kuhuisha na kufuta vibali na leseni za uendeshaji usafiri wa reli;
 • Kuandaa, kupitia na kufuatilia, viwango na kanuni za usalama wa reli;
 • Kuandaa kanuni za maadili kwa watoa huduma wa sekta ndogo ya reli.
 • Kusajili na kuthibitisha wahudumu (dereva na gadi) katika uendeshaji wa treni;
 • Kuidhinisha matumizi ya miundombinu ya reli, mifumo ya usalama na vipengele visivyo vya kawaida vinavyohusiana na usalama wa vyombo vya usafiri kwenye reli;
 • Kutathmini na kutoa ushauri wa maboresho ya utendaji wa sekta ndogo ya reli;
 • Kuthibitisha ubora wa vitendea kazi na miundombinu ya reli;
 • Kuchunguza vyanzo vya ajali na matukio hatarishi ya kiusalama kwenye miundombinu ya reli, vyombo vya usafiri pamoja na mazingira; na
 • Kukuza ushirikiano na nyanja nyingine za usafiri (kama vile barabara).
   
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo