Idara ya Miundombinu ya Reli inatekeleza kazi zifuatazo: -
- Kuandaa, kupitia na kufuatilia utekelezaji wa viwango vya usalama wa miundombinu ya reli;
- Kuandaa, kukagua na kufuatilia uzingatiaji wa kanuni za usalama za miundombinu ya reli;
- Kufuatilia utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa usalama wa miundombinu ya reli;
- Kutoa ushauri kuhusu vipengele vinavyofaa vya usalama kwa mfumo wa udhibiti wa treni;
- Kuchunguza ajali na matukio yanayohusiana na miundombinu ya reli na mazingira;
- Kuthibitisha ubora wa miundombinu ya reli; na
- Kutoa, kuhuisha na kufuta vibali vya matumizi ya miundombinu ya uendeshaji wa reli