Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Mabasi ya masafa Marefu

Amri ya Bodi ya LATRA iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali (Taarifa ya Kawaida Na. 6935), Toleo Na. 47 la tarehe 24 Novemba, 2023 ni kama ifuatavyo:

Kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini, Sura ya 413 imeipa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) jukumu la kupanga na kufanya marejeo ya tozo za huduma ya usafiri ikiwa ni pamoja na nauli za mabasi.

Mamlaka inautangazia umma kuhusu marejeo ya nauli za mabasi ya masafa marefu kama zinavyoonekana kwenye Jedwali hapa chini,

Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu kwa Abiria kwa Kilometa

Daraja la Basi

Hali ya Barabara

Nauli iliyoidhinishwa

Kawaida (Ordinary Bus)

Lami

48.47

Vumbi

53.32

Kati (Semi Luxury Bus)

Lami

67.84

Vumbi

-

 

MAMBO YATAKAYOFUATILIWA NA LATRA

LATRA inawaelekeza watoa huduma wa usafiri wa mabasi ya masafa marefu na mijini (daladala) kuzingatia yafuatayo:

  1. Nauli zinazotozwa zisizidi ambazo zimetolewa kwenye Tangazo hili.
  2. Madereva na wahudumu (makondakta) kuvaa sare safi na nadhifu.
  3. Mtoa huduma kutotoza nauli zaidi ya umbali anaoenda abiria.
  4. Basi liwe safi wakati wote na kupuliza dawa ya kuua wadudu.
  5. Kutumia mfumo unaoruhusu abiria kuchagua kiti na kukata tiketi mtandao.
  6. Kuweka alama kwenye mizigo (luggage tags) kuepuka upotevu.
  7. Kuwatumia madereva waliothibitishwa na LATRA.
  8. Kuhakikisha matumizi ya kitufe cha utambuzi wa dereva (i-button).
  9. Kutokuweka miziki na/au nyimbo na picha (video) zilizo kinyume na maadili ya Kitanzania.
  10. Kuzuia mahubiri ya aina yoyote na kuzuia kufanya biashara ndani ya basi.
  11. Kutunza mazingira kwa kuweka chombo cha kuhifadhi uchafu ndani ya basi.
  12. Kusimama sehemu zenye huduma za kijamii kwa angalau dakika 20.
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo