Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

IDARA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA

Idara inatekeleza kazi zifuatazo;-

 • Kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo ya rasilimali watu;
 • Kusimamia uajiri na kuwapanga wafanyakazi;
 • Kusimamia mfumo wa mishahara na taarifa za rasilimali watu;
 • Kusimamia mchakato wa tathmini ya utendaji wa wafanyakazi na kufuatilia utekelezaji wa matokeo ya tathmini;
 • Kuandaa Makadirio ya Mwaka ya Mishahara ya Wafanyakazi;
 • Kutayarisha na kupitia Sheria na Kanuni za Utumishi, Sera, Mipango ya Utumishi na Muundo wa Mshahara;
 • Kuandaa maslahi ya wastaafu;
 • Kuandaa, kupitia na kuratibu utekelezaji wa Mpango wa kuandaa kiongozi mbadala;
 • Kuratibu na kutekeleza masuala mbalimbali mahala pa kazi;
 • Kusimamia uhusiano mahala pa kazi na masuala ya kinidhamu;
 • Kuratibu Mikutano ya Baraza la Wafanyakazi;
 • Kuratibu masuala ya utawala ya Mamlaka;
 • Kusimamia mali za Mamlaka;
 • Kutayarisha na kupitia Sera, taratibu na miongozo ya utawala;
 • Kusimamia huduma za Masijala;
 • Kusimamia masuala ya ustawi wa wafanyakazi (fidia, afya, usalama, mazishi); na
 • Kuwezesha utoaji wa usalama, usafi wa ofisi, usafiri na huduma za jumla.
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo