Idara inatekeleza kazi zifuatazo;
- Kusimamia shughuli zote za fedha na uhasibu na kuandaa taarifa sahihi za hesabu kwa mujibu wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS);
- Kuandaa na kupitia Sera za Fedha, Kanuni, Miongozo, na Taratibu za Uhasibu
- Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Mamlaka;
- Kufuatilia madeni na kuhakikisha wadaiwa wanalipa ndani wa muda wa unaoruhusiwa;
- Kuandaa bajeti ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo kila mwaka
- Kufuatilia na kushauri kuhusu bajeti ya matumizi ya Mamlaka;
- Kutayarisha Taarifa za Fedha za robo mwaka na mwisho wa mwaka; na
- Kusimamia ukaguzi wa taarifa za fedha za Mamlaka.