Kazi
Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;
- Kuandaa, kupitia na kutekeleza sera zinazohusu fedha, usimamizi wa rasilimali watu na utawala;
- Kuhakikisha matumizi bora na yenye tija ya rasilimali watu na fedha kupitia mipango na bajeti;
- Kuhakikisha kwamba usimamizi wa fedha wa LATRA unaimarishwa, ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa mfumo wa uhasibu unaokubalika;
- Kuhakikisha huduma za ndani zinatolewa kulingana na mahitaji ya mkoa na idara;
- Kuandaa mpango mkakati na mpango wa biashara wa Kurugenzi na kufuatilia utekelezaji wake;
- Kuhakikisha mali za LATRA zinalindwa kwa bima dhidi ya majanga ya aina zote ikiwemo moto, wizi na upotevu wa fedha;
- Kuratibu uandaaji wa taarifa za fedha na kuhakikisha LATRA inakidhi matakwa ya wakaguzi wa nje kila mwaka;
- Kuratibu tathmini ya mwaka ya utendaji wa watumishi katika Mamlaka; na kufanya hivyo kwa Kurugenzi na kusimamia maendeleo ya wafanyakazi.