Idara inatekeleza kazi zifuatazo;:-
- Kutathmini na kupendekeza tozo, viwango na malipo mengine kwa huduma za usafiri ardhini;
- Kufanya tafiti za mara kwa mara za masoko, tathmini na ulinganishaji wa tozo za huduma zinazodhibitiwa kwa ajili ya kuwianisha, utekelezaji wa kanuni za tozo/viwango, kanzidata na usambazaji;
- Kutathmini ushindani wa tozo zinazotozwa katika ukuaji wa sekta na uwezo wa kuzimudu kwa watumiaji;
- Kufuatilia matumizi mabaya ya nafasi katika soko ya watoa huduma wenye uwezo mkubwa, ukiritimba au aina zingine za tabia ya kuhodhi;
- Kuandaa na kupitia upya kanuni za tozo, miongozo na viwango;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uandaaji wa mipango ya biashara kwa watoa huduma; na
- Kubuni na kuendesha mifumo ya usimamizi wa data kuhusu taarifa zilizokusanywa kutoka kwa sekta ndogo inayodhibitiwa