1. Maombi ya Dereva Kusajiliwa
Nyaraka zinazohitajika
a) Leseni ya udereva,
b) Cheti cha taaluma ya udereva kutoka chuo kinachotambulika na Serikali
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, kwenye tovuti www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa usajili wa Dereva au Kondakta,
d) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala za nyaraka zinazohitajika kisha wasilisha maombi,
e) Maombi yatashughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne (24) na mhudumu atapata ankara ya Malipo (Control number),
f) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
Zingatia
Kwa dereva aliyesajiliwa kwenye mfumo na kulipa ada ya usajili, hatalipa ada ya kuthibitishwa pindi atakapowasilisha maombi ya kufanya mtihani.
Gharama
Ada ya usajili TZS.20,000/=
Zingatia
Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (Control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka.
2) Maombi ya Dereva Kuthibitishwa
Nyaraka zinazohitajika
a) Leseni hai ya udereva,
b) Cheti cha taaluma ya udereva kutoka VETA au Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),
c) Cheti cha uthibitisho wa afya kutoka kwenye hospitali inayotambulika na Serikali
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, kwenye tovuti www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa usajili wa Dereva au Kondakta,
d) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala za nyaraka zinazohitajika kisha wasilisha maombi.
e) Maombi yatashughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne (24) na dereva atapata ankara ya Malipo (Control number),
f) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
g) Dereva ataweka nafasi ya kufanya mtihani kwa kuchagua tarehe na muda,
h) Mtihani utasahihishwa na mfumo ( kidigitali),
i) Dereva atapata matokeo ya mtihani kwa njia ya ujumbe mfupi, saa moja baada ya kuwasilisha mtihani wake kwenye mfumo.
j) Dereva aliyefaulu mtihani atapatiwa Cheti baada ya taratibu zote kukamilika.
Zingatia
Hatua za maombi ya kuthibitishwa/kusajiliwa, zitafuatwa na waombaji wanaohuisha vyeti vya uthibitisho baada ya mwombaji kuchagua huduma anayohitaji.
Gharama
a) Ada ya maombi ya Cheti TZS. 10,000/=
b) Ada ya Cheti cha Dereva TZS.10,000/=
Uhai wa Cheti: Miaka miwili
Zingatia
Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (Control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka.
3. Maombi ya Mhudumu Kusajiliwa
Nyaraka zinazohitajika
a) Cheti cha uthibitisho wa afya kutoka hospitali inayotambulika na Serikali.
b) Cheti cha mafunzo ya huduma ya kwanza au huduma bora kwa wateja au mafunzo yoyote kwenye sekta ya usafirishaji
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, kwenye tovuti www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa usajili wa Dereva au mhudumu,
d) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala za nyaraka zinazohitajika kisha wasilisha maombi,
e) Maombi yatashughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne (24) na mhudumu atapata ankara ya Malipo (Control number)
f) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
g) Mhudumu aliyekidhii vigezo atapatiwa kadi ya usajili.
Gharama
a) kusajiliwa TZS. 10,000/=
b) Ada ya kadi ya mhudumu (Crew) TZS.10,000/=
Zingatia
- Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (Control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka
- Bofya hapa kufahamu Vigezo na Masharti ya Mhudumu wa Mabasi aliyesajiliwa na LATRA