Imewekwa: 14 Aug, 2024
Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka ina jukumu la kusajili wahudumu na kuthibitisha madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara.
Kanuni ya 17 ya Kanuni za Uthibitishaji Madereva na Usajili Wahudumu wa Magari ya Biashara za Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini (LATRA) za mwaka 2020, zinamtaka mtu yeyote anayekusudia kufanya kazi ya uhudumu katika gari linalotoa huduma za usafiri kibiashara kusajiliwa na LATRA.