Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(a) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, pamoja na mambo mengine, Mamlaka ina wajibu wa kuhamasisha ushindani wenye ufanisi miongoni mwa watoa huduma zinazodhibitiwa. Katika kutekeleza sehemu ya wajibu huo, Mamlaka iliandaa Tuzo za Wasafirishaji Bora na Salama kwa huduma zilizotolewa kwa mwaka 2023/2024 kupitia mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani.
Lengo la kuanzisha tuzo hizi ni kutambua mchango wa wadau wetu na pia kujenga hamasa ya wao kwa wao kushindana katika kuboresha huduma, kutangaza ubora wa huduma, kupata wateja/abiria zaidi ya waliokosa tuzo na hivyo kuwafanya waliokosa tuzo wajitahidi kuboresha pia nao waje wapate tuzo. Kwa ujumla ni kutambua, kuthamini na kuonesha shukrani kwa wadau wetu. Tumeanza na maeneo machache, miaka ijayo tutaendelea kuboresha na kuenda katika maeneo hata ya kutambu madereva bora na mahiri, makondakta bora na mahiri n.k. Aidha, tutakwenda pia upande wa Reli.