Imewekwa: 22 Nov, 2023
Uamuzi wa Mamlaka wa kutoa mafunzo kwa wahudumu kabla ya kuwasajili unatokana na kukosekana kwa wahudumu waliopata mafunzo rasmi katika sekta ya usafiri ardhini, na pia kukosekana kwa uelewa wa Sheria na Kanuni za huduma za usafiri unaosababisha kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa abiria kuhusu mienendo isiyofaa wahuduma wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hivyo, katika mafunzo haya, mkazo utawekwa kwenye kufahamu Sheria, Taratibu, Kanuni na Kujali Wateja (Customer Care). Kanuni itayosisitizwa ni hii inayohusu Usajili wa Wahudumu ili wajue majukumu yao na pale wasipotimiza majukumu yao wafahamu wanatenda kosa lenye kustahili adhabu